Kuponya

Uponyaji wa kimwili na kiroho ni jambo la muhimu katika maisha ya mkristo imeandikwa Mathayo 4:23 "naye alikuwa akizunnguka katika galilaya yote akifundisha akatika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu."
Uponyaji wa magonjwa sio tu jambo la hali ya juu ambalo Mungu anweza kupeana tu. Imeandikwa Mathayo 9:2 "Natazama wakamletea mtu mwenye kupooza amelala kitandani; naye Yesu alipoiona imani yao alimwambia yule mwenye kupooza jipe mwonyo mkuu mwanangu umesamehewa dhambi zako."

Uponyeji wa mwili unafanyika kwa sababu Mungu anataka kutuponya kiroho. Imeandikwa Mathayo 9:6 "Lakini mpate kujua ya kwamba mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi (amwambia yule mwenye kupooza ) ondoka jitwike kitanda chako uende nyumbani kwako."

Uponyaji wa kiroho ulitolewa na Yesu alipokufa msalabani na kuilipa deni ya dhambi zetu. Imeandikwa Isaiah 53:4-5 "Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amezitwika huzuni zetu lakini tulimdhania ya kuwa amepingwa, amepigwa na Mungu na kuteswa Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona."

Miujiza yauponyaji iliipa ushuja kanisa la mwanzo hapomwanzo wa imani ya Yesu. Imeandikwa Matendo ya mitume 5:16 " Nayo makutano ya miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika wakileta wagonjwa nao walioudhiwa na pepo wachafu nao waote wakaponywa."

Iwapo miujiza ni kipawa cha Mungu lazima tuwe waangalifu kwani shetani anaweza kufanya miujiza pia Imeandikwa Ufunuo 16:14 " hizo ndizo roho za mashetani zifanyazo ishara zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu mwenyezi."

Miujiza haiondoi imani ya mtu Imeandikwa Yohana 20:29-31 "Yesu akamwambia wewe kwa kuwa umeniona umesadiki, wa heri wale wasioona wakasadiki. Basi kuna ishara nyingi alizozifanya Yesu zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ilimpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo mwana wa Mungu na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake."

Kufuata maagizo ya Mungu huleta uponyaji. Imeandikwa Kutoka 15:26 "Akawaambia kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake na kuzishika amri zake mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia wamisiri kwa kuwa mimi ndimi Bwana nikuponyaye."

Mungu aweza kuyaponya magonywa mabaya yanao weza kuleta kifo upesi Imeandikwa Zaburi 107:20 "Hulituma neno lake, huwaponya huwatoa katika maangamizo yao."

Maombi ya imani hufaywa kwa kutakaswa na mafuta huleta uponyaji. Imeandikwa Yakobo 5:14-15 "Mtu wa kwanu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa nao wamwombee na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Nakule kuomba kwa imani kutamwokoa mgojwa yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa."