Home / Masomo ya Biblia / Masengenyo

Masengenyo

Fitina yaweza kuleta nini? Huvunja uhusiano. Imeandikwa Kutoka 23:1 "Usivumushe habari za uongo usitie mkono wako pamoja na mwovu kuwa shahidi wa udhalimu."

Fitina inaumiza na hukaa kama kidonda. Imeandikwa Mithali 25:18, "Mtu ashuhudiaye jirani yake uongo ni nyundo na upanga na mshale mkali."

Fitina hupoteza mda mwema. Imeandikwa 2Wathesalonike 3:11-12 "Maana twasikia yakwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu hawana shuguli za wenyewe lakiniwanajishugulishha na mambo ya wengine basi twaagiza hao na kuwaonya katika Bwana Yesu kristo watenda kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe."

Fitina yaweza kuvunja urafiki. Imeandikwa Methali 16:28 "Mtu shupavu huondokesha fitina na mchongezi huwafarakanisha rafiki."

Imeandikwa Methali 11:13 "Mwenye kitango akisingizia hufunua siri bali mwenye roho ya uwaminifu husitiri mambo."