Mikopo

Twakumbushwa nini kuhusu mkopo?. Imeandikwa Mithali 22:7 "Tajiri humtawala maskini naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye."

Lazima tuwewaangalifu tunapo kopa pesa au mikopo. Imeandikwa Mithali 22:26-27 "Usiwe mmoja wao wawekao rehani au wao wadhamini kwa deni za watu kama huna kitu cha kulipa. Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako!."

Bibilia yasema nini kuhusu malipo ya deni? Imeandikwa, Warumi 13:7-8 "Wapeni wote haki zao mtu wa kodi, kodi mtu wa ushuru, ushuruastahiliye hofu, hofu astahiliye heshima, heshima. Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria."