Mipango

Nivema akupanga mabo mapema. Imeandikwa, Mithal 13:16 Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa bali mpumbavu hueneza upumbavu."
Usiogope weka mipango yako kwa Mungu. Imeandikwa, Mathayo 6:34 "Basi msisumbukie ya kesho kwa kuwa kessho itajisumbukia yenyewe yatosha kwa siku maovu yake."

Tafuta msaada kwak kupanga ya kesho. Imeandikwa. Mithali 15:22 "Pasipo mashauri makusudi hubatilika, bali kwa wingi wa washauri huthibithika."

Panga kwa utaratibu na si kwa haraka. Imeandikwa, Mithali 21:5 "Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji."

Mipango yote sharti iwekwe katika Mungu. Imeandikwa, Yakobo 4:13-16 "Haya basi ninyi msemao, leo au kesho taingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima na kufanya biashara na kupaata faida walakini hamjui yatakayokuwako kesho uzima wenu ni nini? maana ninyi ni mvuke uonekano kwa kitambo, kisha hutoweka badala ya kusema Bwana akipenda tutakuwa hai na kufanya hivi na hivi lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya."

Mtu mwenye busara hupanga ambo yake mapema. Imeandikwa, Luka 14:28-31 "Maana ni nani katika ninyi kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumazizia? asiyeakashidwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema mtu huyu alianza kujenga akawa hana nguvu za kumaliza au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini."

Mungu anampango gani nasi. Imeandikwa, Yeremia 29:11-13 "Maana naya jua mawazo niliyowawazia ninyi, asema Bwana ni mawazo ya amani wala si ya mabaya... Waefeso 1:5, 910 "Kwa kuwa alitangulia kutuchagua ili tufanywe kuwa wanawe kwa njia ya Yesu Kristo sawasawa na urithi wa mapenzi yake akisha kutujulisha siri ya apenzi yake sawasawa na urithi wake alioukusudia katika yeye huyo yani kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia naama katika yeye huyo."