Moyo

Mungu huangalia roho ya mtu na nini kiko katika rohoni. Imeandikwa 1 Samweli 16:1, 7 "Bwana akamwambia Samweli, hata lini utamlilia Sauli ikiwa mimi nimekata asiwamiliki Israeli? ijaze pembe yako mafuta uende nami, nami nitakupeleka kwa Yese Mbethehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe... Lakini Bwana akamwaambia Samweli usimtazame uso wake, wala urefu wakimo chake; kwa maaana mimi nimemkataa Bwana haangali kama binadamu aangaliavyo maana binadamu huitazama sura ya nje bali Bwana huutazama moyo."

Mioyo inahitaji kusafiswa imeandikwa Zaburi 51:10 "Ee Mungu uniumbiye moyo safi, uifanye upia roho iliyotulia ndani yangu."

Mioyo yetu itatulia tunapojua yakuwa mambo yote yako katika mikononi mwa Mungu. Imeandikwa 1Yohana 3:19-20 "Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote."

Sharti tu utowe moyo wetu wote kweke Mungu. Imeandikwa Warumi 6:17 " Laki Mungu na ashukuriwe kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mlitii kwa mioyo ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake."