Mvinyo

Neno la Mungu latueleza vipi kuhusu ulevi Imeandikwa Mithali 20:1Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima."

Kwa nini mvinyo una hatarisha Imeandikwa waefeso 5:18 "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe na roho."

Kwa nini wafalme na viongozi hawapaswi kunywa mvinyo? Imeandikwa Midhali 31:4-5 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; wala haifai wakuu, waseme kiwapi kileo? Wasije wakanywa nakuisahau sheria, na kuipoteza hukumu ya mtu aliye taabuni."

Imeandikwa Wagalatia 5:19-21Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya uwasherati, ushafu, ufisadi ibada ya sanamu uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, namambo yanayo fanana na hayo katika hayo na waambia mapema, kama nilivyo kwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya njinsi hiyo hawatauridhi ufalme wa Mungu."

Nimatokeo ngani tuna pata kutokana na ulevi na ulafi mwingi imeandikwa Medhali 23:20-21 "Sikia mwanangu uwena hekima, Na kuongoza moyo wako uwe na hekima, na uongoza moyo wako katika njia njema. usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; miongoni mwao walao nyama kwa pupa. kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, na utepetevu humvika mtu nguo mbovu."

Pombe ina wadhuru kivipi wanao itumia? imeandikwa Medhali 23:29-35 "Ninani apigaye yowe? ninani aliya, ole? ninani mwenye ugomvi? ninani mwenye mnguno? Ni nani mwenye jeraha zisizo na sababu? ni nani aliye na macho mekundu? niwale wakaao kwenye mvinyo; waenda kutafuta divai iliyochanganyika usiitazame mvinyo iwapo nyekundu; iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; mwisho wake huuma kama nyoka; huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni. Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asingizie juu ya mlingoti. utasema wamenishapa wala sikuumia; wamenipiga wala sina habari; nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena."
Imeandikwa Isaya 65:8, "Mwana asema hivi kamavile divai mpya ipatikanayo katika kishala, na mtu mmoja husema, msikiharibu kwamaana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyo tenda watumishi wangu, ili nisi waharibu wote."