Ndoa

Je! Bibilia ya funza nini kuhusu ndoa?. Imeandikwa, Mathayo 19:5-6 "Asema kwasabu hiyo mtu atamwacha babye na mamaye ataambatana na mkewe na hao wawili watakua mwili mmoja? hata wamekua si wawili tena bali mwili mmoja basi aliowaunganisha Mungu mwanadamu asiwatenganishe."

Je! waume wawatendeaje wake zao?. Imeandikwa, Waefeso 5:25-28 "Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wal kunyazi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume na kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe mewenyewe."

Waume wa waheshimu wake zao. Imeandikwa, 1Petro 3:7 "Kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa akili na kupa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu, na kama waridhi pamoja wa neema ya uzima kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe."

Je wake nao wake na waume zao vipi?. Imeandikwa, Waefeso 5:22-24 "Enyi wake watiini waume zenu kama kutii Bwana wetu kwa maana mume ni kishwa cha mkewe kama Kristo naye nikichwa cha kanisa, naye nimwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo."

Je inamaanisha ya kuwa wake wafanye kila jambo? Asha!. Imeandikwa, Waefeso 5:21 "Hali mnanyenyekea katika kicho cha Kristo."

Je tumeagizwa kutoa kupigana kwa mke na mme. Imeandikwa, Wakolosai 3:19 "Ninyi waume, wapendeni waume zenu, msiwe na uchungu nao."

Kuwa na ndoa njema nivema kutatua mafaragano au kutoelewana mara moja. Imeandikwa, Waefeso 4:26 "Mwea na hasira ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka."

Fanya ndao yako ikuwe kwa umoja na kuelewana. Imeandikwa, Waefeso 4:2-3 "Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo na kujitahidi kuuhifadhi umoja kwa Roho katika kifungo cha amani."

Je! watu wapaswa kuiona vipi ndoa. Imeandikwa, Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi kwa maana washerati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu."

Kwa amri gani Mungu ameilinda ndoa. Imeandikwa, Kutoka 20:14, 17 "Usizini". Usitamani nyumba ya jirani yako usitamani nyumba ya jirani yako..."

Je Mungu ameamua kuvunja ndoa katika hali gani? Imeandikwa, Mathayo 5:32 "Lakini mimi nawaambia, kila mtu amwachaye mkewe isipokua kwa habari ya uasherati amefanya kuwa mzinzi, na mtu akimwoa yule aliyeachwa azini."

Je ndoa ikae kwa mda gani. Imeandkwa, Warumi 7:2 "Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokua hai, bali akifa yule mume amefunguliwa ilesheria ya mume."

Je tumeagizwa kumuoa nani? Imeandikwa 2Wakorintho 6:14 "Msifungwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa kwa maana kuna urafiki gani kati ya haki na uasi? tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?."

Malazi yamebarikiwa na Mungu wakatika ndoa. Imeandikwa, Mithali 5:18-19 "Chemchemi yako ibarikiwe nawe umfurahiye mke waujana wako ni alaya apendaye na paa apendezaye."