Pumziko

Wakati mambo yamekua magumu fedha, familia na maisha yamezidi kukusonga kuna jibu. Imeandikwa Mathayo 11:28-30 "Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha jitieni nira yangu, mjifunze kwangu kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi."

Mungu ametupa mfana mwema wa kupumzika. Imeandikwa, Mwanzo 2:3 "Mungu akaibariki siku ya saba akaitakasa kwa sababu katiak siku hiyo Mungu alistarehe akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya."

Kupumzika hufanya kumwabudu Mungu kuwa wa kweli. Imeandikwa, Kutoka 20:8-11 "Ikumbuke siku ya sabato uitakase siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako wala mjakazi wako wala mnyama wako wa kufuga wala mgeni aliye ndani ya malango yako. maana kwa siku sita Mungu alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba kwa hiyo Bwana Mungu akaibariki siku ya sabatu akaitakasa."

Kupumzika ni zawadi kutoka kwa Mungu na ipo katiaka pango wa Mungu. Imeandikwa, Waebrania 4:9-11 "Bali imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu kwa sababu yeye aliyeingia katika raha yake ametarehe mwenyewe katiaka kazi yake kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. basi na tufanye bidii kuingia katiaka raha ile ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka k w amfano uo huo wa kuasi."

Kuna mapumziko katika wokovu. Imeandikwa, Isaya 30:15 "... Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa......"