Shatani

Dhambi ilitoka wapi? kwake shetani. Imeandikwa, 1Yohana 3:8 "Atendaye dhambi ni wa ibilisi kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za Ibilisi."

Shetani amekua mwongo na muuaji kwa mda gani?. Imeandikwa, Yohana 8:44 "Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi na tamaa za baba zenu ndizo mpendazo kuzitenda. yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo wal hakusimama katika kweli kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa sababu yeye ni mwongo na baba wa huo."

Shetani alitoka wapi?. Imeandikwa, Ufunuo 12:7-9 "Kulikua na vita mbinguni, Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni yule joka akatupwa yule mkubwa, nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye."

Je shetani aliumbwa akiwa mwene dhambi?. Asha! aliumbwa akiwa mkamilifu na uwezo wa kuchagua. Imeandikwa, Ezekieli 28:15 "Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa hata uovu ulipoonekana ndani yako."

Nini kilicho mfanya shetani kuanguka? Imeandikwa, Ezekieli 28:17 "Moyo wako uliinika kwa sababu ya uzuri wako umeiharibi hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako ni mekutupa chini ni mekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama."

Shetani alijulikana kama Lusifa, alitka kuwa kama Mungu. Imeandikwa, Isaya 14:12-14 "Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni Ewe nyota ya alfajiri mwana wa asubuhi jinsi ulivyo katwa kabisa Ewe uliyewaangusha mataifa nawe ulisema moyoni mwako nitapanda mpaka mbinguni nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu nami nitakaa katika mlima wa makutano katika pande za mwisho za kaskazini, Nitapata kupita viun o vya mawingu nitafanana na yeye aliye juu."

Tofauti ya shetani na kiburi chake Yesu alikua na roho ya ainagani? Imeandikwa, Wafilipi 2:6-8 "Ambaye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho bali alijifanya kuwa hanautukufu akatwa namna ya mtumwa akawa anamfano wa mwanadamu tena alipoonekana anaumbo kama wa mwandamu alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti naam mauti ya msalaba."

Uwezo washetani waleta vita. Imeandikwa, Waefeso 6:11Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za sheteni."

Shetani alimjaribu Yesu. Imeandikwa, Mathayo 4:1 "Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na Ibilisi."

Shetani ameshindwa. Imeandikwa, Yakobo 4:7 "Basi mtiini Mungu, mpingeni Shetani naye atawakimbia."