Home / Masomo ya Biblia / Uaminifu

Uaminifu

Mungu anahitaji sisi tuwe waaminifu. Imeandikwa, Zaburi 51:6 "Tazama wapendezwa na kweli iliyo moyoni nawe utanijulisha hekima kwa siri."

Kutokuwa mwaminifu kwa mwezio ya weza kudhuru mtu. Imeandikwa Mithali 25:18 "Mtu ashuhudiaye jirani yake uongo ni nyundo na upanga, na mshale mkali."

Mungu hakubali kuwa na biashara isiyo ya kweli. Imeandikwa, Mithali 20:23 "Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa Mungu tena mizani ya hila si njema."

Uwemwaninifu. Imeandikwa, 1Wathesalonike 2:3 "Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu wala ya uchafu wala ya hila." 2Wakorintho 8:21 yasema "Tukitangulia kufikiri yaliyo mema si mbele za Bwana tu ila na mbele za wanadamu."

Uaminifu ukokatika amri bili. Imeandikwa, Kutoka 20:15-16 "Usiibe. Usimshuhudiye jirani yako uongo."

Viongozi wanawaheshimu wale wanao sema kweli. meandikwa, Mithali 16:13 "Midomo ya haki ni furaha ya wafalme nao humpenda yeye asmaye yalio sawa."

Ukweli ni wadhamani kuu. Imeandikwa, Mithali 28:23 "Amkemeaye mwezake hatimaye atabata kibali. zaidi ya mtu ajipendezaye kwa ulimi wake."

Watoto wa wazazi waaminifu wamebarikiwa. Imeandikwa, Mithali 20:7 "Mwenye haki aendaye katika unyofu wake watoto wake wabarikiwa baada yake."

Ongea kweli. Imeandikwa. Mithali 12:13-14 "Katika kosa kwa mdomo kuna mtego kwa mbaya bali mwenye haki atatoka kwenye taabu. Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake na atarudishiwa matendo ya mikono yake."

Uongo utadumu kwa mda mfupi tu. Imeandikwa, Mithali 20:17 "Chakula cha uongo nikitamu kwa mtu lakini halafu kinywa chake kitajachangarawe."

Utajiri wa uongo haudumu, Imeandikwa, Mithali 21:6 "Kupata akiba ya mali ya ulimi wa uongo n moshi upeperushwao ni kutafuta mauti."

Fanya kwa njiya ya Mungu. Imeandikwa, Mithali 11:1 "Mizani ya hada ni chukizo kwa Bwana bali vipimo vilivyosawasawa humpendeza."

Mungu hudhamani uaminifu. Imeandikwa, Mithali 21:3 "Kutenda haki na hukumu humpendeza Bwana kuliko kutoa sadaka."