Home / Masomo ya Biblia / Ugama, Kukiri

Ugama, Kukiri

Ungamo hufungua njia ya msamaha. Imeandikwa katika 1Yohana 1:9 " Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolea dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."

Ungamo huandaa mazingira ya ibada. Imeandikwa katika Nehemia 9:3 "Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha torati ya BWANA Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakangama, wakamwabudu BWANA, Mungu wao."

Maungamo huandaa njia ya mapatano na ushirika. Imeandikwa katika Yakobo 5:16 "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii."

Kuungama hufanya mafanikio yawezekane. Imeandikwa katika Mithali 28:13 "Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."