Ukristo

Mtu aweza kuwa Mkristo vipi? Kwa njia ya kuwa na uhusiano na Mungu. Imeandikwa katika Yohana 17:3 "Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma."

Kuwa Mkristo ni kuikubali injili. Imeandikwa katika Matendo ya mitume 2:37-38 "Waliposikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu."

Ukristo ni wa mtu binfsi na halikadhalika wa kila mtu Imeandikwa katika Warumi 10:8-10 "Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, Katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani ni lile neno la imani tulihubirilo. Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinyua chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako yakuwa mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinyua mtu hukiri hata kupata wokovu."

Ni jambo la maana mtu akisema ana amini liwe tu sio wazo lakini ni zaidi ya wazo au shauri ni kuamini kwa moyo wako wote, pia unahitaji Roho mtakatifu akiishi ndani yako kukuwezesha kuishi maisha ya kikristo. Imeandikwa katika Warumi 8:9 "Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mwili bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake."

Ukristo wahitaji uchambuzi wa kweli wa neno la Mungu. Imeandikwa Luka 1:3-4 "Nimeona vema mimi nami kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu Thofilo mtukufu, upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa."