Mungu ametuahidi kuwapamoja nasi katika ukuwaji wetu wa kiroho. Imeandikwa, Wafilipi 1:6 "nami niliaminilo ndilo hili ya kwamba yeye aliye anza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu."
Yesu ndiye mwanzo wa ukuwaji wa kiroho. Imeandikwa, Wakolosai 2:6-7 "Basi kama mlivyo pokea Yesu Kristo Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye, wenye shina na wenye kujengwa katika yeye mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani."