Umbo

Usiwahukumu wengine kwa mwonekano. Kumbuka Mungu hutizama ndani zaidi ya hapo. Imo katika Bibia, 1Samweli 16:7 "Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usitazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwe maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama vile binadamu aagaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo."

Ushuhuda wetu umeungwa pamoja na mwonekano wetu. Imo katika Biblia, 1Timotheo 2:9-10 "Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele wala kwa dhahabu na lulu wala kwa nguo za thamani bali kwa matendo mema kama ipasavyo wanawake wanao ukiri uchaji wa Mungu." 1 Petro 3:3, 4, "Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje yaani kusuka nywele; na kujitia dhahabu na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana kama mapambo yasiyoharibika; yaani roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu."