Unabii

Nabii haji kwake bali kwa kutumwa na Mungu. Imeandikwa, 2Petro 1:21 "Maana unbii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu walinena yaliyo toka kwa Mungu wakiongozwa na Roho mtakatifu."

Unabii hueleza yatakayo tokea siku zijazo. Imeandikwa, Isaya 42:9 " Tazama mambo ya kwa nza yamekuwa nami nayahubiri mambo mapya lkabla hayajatokea nawapasheni habari zake."

Mungu ametufunulia mipango yake kupitia kwa manabii. Imeandikwa, Amosi 3:7 "Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote bila kiwafunulia watumishi wake manabii siri yake."