Upole

Viongozi wa makanisa nivema wakionyesha upole imeandikwa 1Wathesalonike 2:6-7 "Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu wala kwenu wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe."

Fundisha kwa upole. Imeandikwa 2Timotheo 2:24 "Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi bali kuwa mwana kwa watu wote awezaye kumfudisha mvumilivu."

Upole ni onyesho la hekima imeandikwa Yakobo 3:17 "Lakini hekima itokayo juu kwanza ni safi tena yenye amani ya upole tayari kusikiliza maneno ya watu imejaa rehema na matunda mema haina fitina haina unafiki."