Upweke

Mungu ndiye rafirki wa kudumu. Imeandikwa Kumbukumbu la torati 31:8 "Naye Bwana yeye ndiye atakayekutangulia atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike."

Mungu atakuwa nawe wakati wapendwa wako wamekuacha kwa kifo. Imeandikwa, Zaburi 23:4 "Naam nijapopita kati ya ponde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami gongo lako na fimbo yako vyanifariji."

Mungu hatatucha hata wazazi wetu wakitukana na kutuacha. Imeandikwa, Zaburi 27:10 "Baba yangu na mama ya ngu wemeniacha, bali Bwana atanikaribisha kwake."

Mungu hatatuacha kama yatima. Imeandikwa, Yohana 14:18 "Sitawaacha ninyi yatima naja kwenu."

Hatu upweke. Imeandikwa, Waebrania 13:5 "Msiwe na tabia ya kupenda fedha mweradhi na vitu mlivyo navyo kwa kuwa yeye mwenyewe amesema sitakupungukia kabisa wala sita kuacha kabisa."