Urahisi

Kwaurahisi wa injili watoto wafahamu anayo sema Yesu. Imeandikwa, Mathayo 11:25 "Wakati ule Yesu akajibu, nakushukuru baba na Bwana wa mbingu na nchi kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili ukawafunulia watoto wachanga."

Twampata Mungu kwa urahisi kwa kuamini tu. Imeandikwa, 1Wakorintho 1:21 "Kwa maana katika hekima ya Mungu dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa."

Uzuri wandani nikuwa urahisi. Imeandikwa, 1Petro 3:3-4. "Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje yani kusuka nywele na kujitia dhabu na kujivalia mavazi bali kuwe utuwamoyoni usioonekana katika mapambo yasiyoharibika yani roho ya upole na utulivu, iliyo ya dhamani kuu mbele za Mungu."

1Timotheo 2:9, 10, yasema "Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri pamoja na adabu nzuri na moyo wa kiasi si kwa kusuka nywele wala kwa dhahabu na lulu wala kwa nguo za thamani bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu."