Urembo

Je? ni urembo upi unaofaa? Imeandikwa katika 1Petro 3:3-4 "Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, yaani kusuka nywele na kujitia dhahabu, nakuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za MUNGU."

Urembo wa kweli sio wa kujipenda au kujivuna. Imeandikwa katika 1Timotheo 2:9-10 "Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri pamoja na adabu nzuri na moyo wa kiasi si kwa kusuka nywele wala kwa dhahabu na lulu wala kwa nguo za thamani bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa MUNGU."

Urembo unapatika kwake Mungu, imeandikwa katika Zaburi 90:17 "Na uzuri wa BWANA, Mungu wetu uwe juu yetu..."