Home / Masomo ya Biblia / Utakatifu

Utakatifu

Utakatifu wa Mungu ndio kipeo chetu chakuishi maisha ya utakatifu imeandikwa 1 Petro 1:15 "Bali kama yeye aliyewaita alivyo matakatifu ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote."

Utukufu wa Mungu hauwezi kuwa pamoja na dhambi. imeandikwa Isaya 59:2 "Lakini waovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kusikia."

Utakatifu ni kipawa cha neema ya Mungu. Imeandikwa Kutoka 19:5-6 "Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kuishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu maana ndunia yote pia ni mali yangu ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa kuhani na taifa takatifu hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana waisraeli."

Utakatifu hukuwa kwa kuitii neno la Mungu. Imeandikwa Yohana 17:17 "Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli."