Home / Masomo ya Biblia / Uvuguvugu

Uvuguvugu

Mungu ana chukia watu wasio na msimamo katika hali ya kiroho imeandikwa Ufunuo 3:15-16 "Nayajua matendo yako yakuwa hu baridi wala hu moto ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvungu, wala hu baridi wala moto nitakutapika utoke katika kinywa changu."

Usiwe mvuguvugu katika msimamo wako imeandikwa Isaya 50:7 "Maana Bwana mungu atanisaidia kwa sababu hiyo sikutahayari kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua yakuwa sitaona haya."

Usichanganyikiwe na mamo yasio na mwelekeo imeandikwa Yeremia 32:38-39 "Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa mungu wao nami nitawapa moyo mmoja na njia moja wapate kunicha siku zote kwa mema yao na ya watoto wao baada yao."

Katashauri kumcha mungu na kumtumikia imeandikwa Yoshua 24:15 "Nanyi kama mkiona nivibaya kumtumikia Bwana changueni hivi leo mtakaye mtumikia kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu wali itumikia ng'ambo ya mto au kwamba ni miungu ya wale waamori ambao mnakaa katika nchi yao lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana."