Zaka

Kabla ya kutumia pesa zako au mazao yako tunapaswa kumpa Mungu sehemu yake kwanza. Imeandikwa, Mithali 3:9 "Mheshimu Bwana Mungu wako kwa mali yako na kwa malimbuko ya mazao yako yote."

Je? ni sehemu gani ya mapato yetu twapaswa kutoa zaka. Imeandikwa, Mambo ya walawi 27:30 "Tena zaka yote ya nchi, kama ni begu ya nchi ni ya Bwana, ni takatifu kwa Bwana."

Zako ya tuonyesha kuwa Mungu awe wa kwanza katika maisha yetu. Imeandikwa, Kumbukumbu ya torati 14:22-23 "Usiashe kutoa zaka ya fungu la kumi katika maogeo yote ya mbegu zako yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako mahali atakapochagua apakalishe jina lake zaka ya nafaka yako na wazaliwa wakwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako daima."

Je zaka ilitumikaje katika wakati wa wana waisraeli. Imeadikwa, Hesabu 18:21 "Na wana wa lawi nime wapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao badala ya huo utumishi, wautumikao maana ni huo utumishi wa hema ya kukutania."

Kristo alisisitiza utowaji wa zaka. Imeandikwa, Mathayo 23:23 "Ole wenu waandishi na wafarisayo wanafiki kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira lakini mmeasha mambo makuu ya sheria yani adili ya rehema, na rehema, na imani; hayo imewepesa kuyafanya, wala yale mengine masiyaashe."

Paulo asemaje kuhusu kusaidia injili?. Imeandikwa, 1Wakorintho 9:13-14 "Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu na wale waihudumio madhababu huwa na fungu lao katika madhahabu? na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwaba wale waihubiriyo injili wapate ridhiki kwa hiyo injili."

Je? sheria ya kutoa zaka ya patikana wapi. Imeandikwa, Zaburi 24:1 "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana. Dunia na wote wakao ndani yake."

mali yatoka wapi?. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 8:18 "Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri ili alifanye imara agano lake alilowapa zako kama hivi leo."

Bali na zaka twaulizwa mkuleata nini katia malango ya hekalu?. Imeandikwa, Zaburi 96:8 "Mpeni Bwana utukufu wa jina lake leteni sadaka mkaziingie nyua zake."

Mungu anatwambia kuwa tumewiba kwa zaka na sadaka. Imeandikwa, malaki 3:8 "Je mwanadamu atamwibia Mungu? lakini ninyi mwasema tumekuibia kwa namna gani? mmeniibia zaka na dhabihu."

Je! Mungu asema tumjaribu kwa namna gani? Imeandikwa, Malaki 3:10 "Leteni zaka kamili ghalani ili kiwepo chakula kingi nyumbani yangu mkanijaribu kwa njia hiyo asema Bwan wamajeshi mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbiguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha au la."

Peana kwa furaha kwakuwa unamfurahisha Mungu. Imeandikwa, 2Wakorintho 9:7 "Kila mtu na atende kama alivyokusudiwa moyoni mwake si kwa huzuni wala si kwa lazima maana Munug humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu."

Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 16:17 "Kila mtu atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya Bwana Mungu wako, alivyokupa."