Hasira

Mtu mwenye hasira ni mpumbavu. Imo katika Biblia, Mhubiri 7:9 "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu." Mithali 19:11 na 16:32." Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; nayo ni fahari ya kusamehe makosa." 16:32 "Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji."

Iachilie hasira kwa upesi. Imo katika Biblia, Waefeso 4:26-27, "Mwe na hasira wala msitende dhambi; jua lisichwe na uchingu wenu bado hujawatoka wala msimpe ibilisi nafasi."

Usirudishe hasira kwa mtu ambaye amekutenda ovu, Imo katika Biblia, 1Petro 3:9 "Watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki kwa sababu hiyo ndiyo mliyoitwa ili mrithi baraka."

Hasira huleta ugomvi. Imo katika Biblia, Mithali 30:33 "Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Nakupiga pua huleta damu; kathalika kuchoshea hasira hutokeza ugomvi."