Hekima

Hekima huja wakati tupomuliza Mungu hekima. Imeandikwa, 1Wafalme 3:9 "Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili ni wahukumu watu wako na kupambanua mema na mabaya maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi."

Mungu hutupa hekima jinsi ya kushi na katika maisha yetu. Imeandikwa Zaburi 119:97-98, "Sheria yako naipenda mno ajabu Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu kwa maana ninayo siku zote."

Mwamini Mungu naye atakufanya kuwana hekima. Imeandikwa Mithali 1:7 "Kumcha Bwana nichanzo cha maarifa bali wapumbavu hudharau hekima na adabu."

Maarifa au hekima ni kuweza kuona maisha katika macho ya Mungu na kuweza kufanya asemayo Mungu. Imeandikwa, Mhubiri 8:1 "Ni nani aliye kama mwenye hekima. Naye ni nani ajuaye kufasiri neno hekima ya mtu humng'ariza uso wake na ugumu wa uso wake hubadilika."

Twakuwa wenye hekima tunapokuwa katika Kristo. Imeandikwa, Luka 2:40 "Yule mtoto akakuwa akaongezeka nguvu amejaa hekima na neema ya Mungu ikiwa juu yake."

Twaweza kumuliza Mungu atupe hekima katika uchaguzi wetu wa maisha. Imeandikwa Yakobo 1:5 "Lakini mtu wakwenu akipungukiwa na hekima na aobe dua kwa Mungu awapaye wote kwa ukarimu wala hakemei naye atawapatia."