Heshima

Twastahili kumpa Mungu heshima kuu Imeandikwa, Kutoka 3:5 "Naye akasema usikaribie hapa vua viatu vyako miguuni mwako maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu."

Nivema kuwapa heshima viongozi wetu. Imeandikwa, 1Samueli 24:5-6 "Lakini halafu moyo wake Daudi ukamchoma kwa sababu aekata upindo wa wa vazi lake Sauli. Akawaambia watu wake hasha nisimtende bwana wangu masihi wa Bwana neno hili kuunyosha mkono wangu juu yake kwa maana yeye ni masihi wa Bwana."

Nivema kuwapa watu wengine heshima. Ieandikwa, 1Petro 2:17 "Waheshimuni watu wote wapendeni ndugu. Mcheni Mungu mpeni heshima mfalme."

Tuwaheshimu wazee au watu wazima. Imeandikwa, Mambo ya walawi 19:32 "Mwondokeeni mtu mwenye vi heshimunu uso wa mtu mzee nawe mche Mungu, wako mimi ndimi Bwana."