Jehanam

Mshara wa dhambi ni mauti sio kuteswa milele na milele. Imeandikwa, Warumi 6:23 "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Munug ni uzima wa milele katiaka Kristo Yesu Bwana wetu."

Waovu wataangamia. Imeandikwa, Zaburi37:20 "Bali wasio haki watapotea nao wamchukia Bwana watatoweka kama uzuri wamashamba kama moshi watatoweka."

Waovu waungua na hakuna litakalo baki kwao. Imeandikwa, Malaki 4:1Kwa maana angalieni ile siku inakuja inawaka kama tanuru na watu wote wenye kiburi nao waote watendao uovu watakuwa makapi na siku ile inayokuja itawateketeza asema Bwana wa majeshi hata haitawachia china wala tawi."

Imeandikwa, Mathayo 25:46 "Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele."

Sodoma na Gomora waliteketezwa na moto wa milele bali sasa haaunugi katika ule moto. Imeandikwa, Yuda 1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyo kuwa kando -kando walio fuata uasherati kwa jinsi moja na hawa wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili imewekwa kwa dalili wakiadhibiwa katika moto wa milele."

Moto hautazimwa kwa maji au kwa lolote lakinim wakati umekwisha teketeza yote utazimika. Imeandikwa, Mathayo 3:12 "Ambaye pepeto lake limkononi mwake naye atausafisha nasa uwanda wake na kuikusanya ngano yake galani bali makapi yata teketezwa kwa moto usiozimika." Yeremia 17:27 yasema Lakini kama hamtaki kunisikiliza kuitakaza siku ya Sabato, kutokuchuka mzigo na kuingia malngo ya Yerusalemu siku ya Sabato basi nitawasha moto malangoni mwake na utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu wala hautazimika."

Dunia yote itasafishwa kwa moto. Imeandikwa 2 Petro 3:10 "Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi Katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu na viumbe vyaasili vitaunguzwa na kufumuliwa na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea."

Ni nani watakao kuwa katika ziwa la moto? Imeandikwa. Ufunuo 20:15 "Naiwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikw akatika kitabu cha uzima, alitupwa katika kile kiziwa cha moto."

Jehanam ni tukio si mahali. Imeandikwa, Ufunuo 20:9 "Wakaipanda juu ya upana upana wa nchi wakizingira kambi ya watakatifu na mji huo uliopendwa moto ukashuka kutoka mbinguni ukawala."