Kanisa

Kanisa ni nini? siyo jengo bali ni wale waliomo ndani yake. Imo katika Biblia, Matendo ya mitume 17:24 "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa bingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono."

Kanisa ni watu wanao amini Imeandikwa wefeso 2:21 "Katika yeye jingo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika bwana." 1Wakorintho 3:16 "Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na yakuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?.

Kazi ya kanisa ni ipi? Kanisa inaeneza ijili Imeandikwa 2 Timotheo 4:2 "Lihubiri neno uwe tayari wakati ufaao na wakati usiokufaa karipia kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho."

Kanisa limepewa maagizo na Mungu. Imeandikwa katika Waefeso 4:12 "Kwa kusudi kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe."

Kila mshiriki ana jukumu maalum. Imeandikwa katika 1 Wakorintho 12:13, "Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja kwamba tu wayahudi au kwamba tu wayunani ikawa tu watumwa au ukawa tu huru nasi tulinyweshwa Roho mmoja."

Wakristo tu wafariji wenzetu Imeandikwa Waebrania 10:25 "Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia."