Home / Masomo ya Biblia / Kutafakari

Kutafakari

Kutafakari kwa mkristo kuna maana gani, nijambo la uaminifu kwa Mungu. Imeandikwa, Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliyo andikwa humo maana ndipo utakapo ifanikisha njia yako kasha ndipo utakapo sitawi sana."

Kutafakari kwa wakristo ni kuangalia kuwa unaenenda kulingana na mipango ya Mungu. Imeandikwa, Zaburi 1:2 "Bali sheria ya Bwana ndiyo ipendezayo na sheri yake huitafakari mchana na usiku.".

Yesu ametupa mfano bora jinsi ya kutafakari na maombi. Imeandikwa, Luka 5:16 "Lakini yeye alikuwa akijiepua akaenda mahali pasipo kuwa na watu, akaomba."

Kutafakari yatoka katika kuelemika. Imeandikwa, 2Timotheo 2:7 "Yafahamu sana hayo nisemayo kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote."