Maisha

Nini kinasho fanya maisha kuwa ya dhamani? Watu wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Imeandikwa, Mwanzo 9:6 "Atakayemwanga damu ya mwanadamu damu yake huyo itamwangwa na mwanadamu maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu."

Kila mda katika maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu. Imeandikwa, Zaburi 39:4 "Bwana unijulishe mwisho wangu na kiasi sha siku zangu ni kiasi gani nijue jinsi nilivyo dhaifu."

Kuishi maisha tukijia tutaishi milele huleta dhamana katika maisha haya. Imeandikwa, Zaburi 90:12 "Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu tujipatie moyo wa hekima."

Tukiishi maisha ya kujinyima kwa sababu ya imani yetu kwa Mungu hufanya maisha kuwa bora. Imeandikwa, "Marko 8:35 "Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili huyu ataisalimisha."

Maisha ya kiroho ni ya kujinyima. Imeandikwa, Luka 9:25 "Kwa kuwa ya mfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote kama akijiangamiza au kujipoteza mwenyewe?"

Maisha ya kiroho ni kuw na uhusiano na Mungu na inapatika kwake. Imeandikwa, Warumi 6:5-7 "Kwa maana kama mlivyounganikanaye katika mfano wa mauti yake kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake, mkijua neno hili kuwa utu wetu wakale ulisulubishwa pamoja naye ilimwili wadhambi ubatilike tusitumikie dhambi tena kwa kuwa yeye aliyekufa yeye amehesabiwa haki mbali na dhambi." Yohana 14:6 yasema "Yesu akamwambia mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi."