Home / Masomo ya Biblia / Maisha mapya

Maisha mapya

Tunapo mkubali Yesu kama mwokozi wetu tuna anzamaisha mapya. Imeandikwa, Waefeso 4:21-24. "Ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye kama kweli ilivyo katika Yesu, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuta tamaa zenye kudanganya na mfanywe wapia katika roho ya nia zenu, mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli." 2 Wakorintho 5:17 yasema "Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya yakaze yamepita tazama yamekuwa mapya."

Maisha mapya yapatikana katika kristo na kifo chake. Imeandikwa, Warumi 6:5 "Kwa maana kama mlivyouganika naye katika mfano wa mauti yake kadhalika mtauganika kwa mfano wa kufufuliwa kwake."

Maisha mapya yaleta uhuru katika dhambi. Imeandikwa, Wakolosai 2:13-14 "Nanyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake ilivyokuwa na uadui kwetu akaiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."