Mapepo ni malaika walio anguka au walio asi kule mbinguni na yule shetani Imeandikwa Ufunuo 12:9 "Yule joka akatupwa, yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye."
Mapepo wana nguvu sana lakini Mungu amewapa kadiri au kipimo. imeandikwa Marko 1:27 "Wakashangaa wote hata wakaulizana wakisema ni nini hii ni elimu mpya! maana kwakuwa wa amuru hata pepo washafu nao wamtii!".
Jesu ananguvu kuliko mashetani imeandikwa Luka 4:35-36 "Yesu akamkemea akisema fumba kinywa mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno, Mshangao ukawashika wote wakasemezana wakisema ni neno gani hili maana waamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu nao hutoka."
Mashetani wako je leo? adui haonekani lakini vuta viko imeandikwa Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
Tukinyenyekea mbele za mungu yule shetani atatoroka imeandikwa Yakobo 4:7 "Basi mtii mungu, mpingeni shetani naye atawakimbia."