Home / Masomo ya Biblia / Matumaini

Matumaini

Tumaini huja wakati unapokumbuka yale ambayo Mungu amekutendea. Imeandikwa. Warumi 5:1-2 " Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii amabayo mnasismama ndani yake na kufufrahi katika tumaini la utukufu wa Mungu."

Unapo vunjika moyo kuwa na imani kwa Mungu. Imeandikwa Zaburi 42:11 "Nafsi yangu kwa nini kuinama, na kufadhaika ndani yangu? umtumaini Mungu kwa maana nitakuja kumsifu, aliye afya ya uso wangu na Mungu wangu."

Imani husababisha mambo mema. imeandikwa. Wakolosai 1:5 "Kwasababu ya tumaini mlilowekewa akiba Mbinguni ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya injili."

Tumaini hukuwa wakati tunapo kumbuka ufufuo. Imeandikwa. 1Wathesalonike 4:13 "Lakini ndugu, hatutaki msijue habari za waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasiso na tumaini."

Lazima utumie moyo wako kutafuta imani. Imeandikwa Waefeso1:18 "Masho ya mioyo yenu yatiwe nuru mjuwe tumaini la mwito wake jinsi lilivyo na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo."