Home / Masomo ya Biblia / Mbinguni

Mbinguni

Je biblia yasemaje kuhusu mbinguni? Imeandikwa, Yohana 14:2-3 "Nyumbani mwa baba yangu mna makao mengi kama sivyoningaliwaambia maana naenda kuwaandalia mahali basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali nitakujatena niwakaribishe kwangu ili nilipo nanyi mwepo."

Mbinguni ni mahali ambapo hatuwezi kufafanua kwa mafikara yetu. Imeandikwa 1Wakorintho 2:9 "Lakini kama ilivyoandikwa mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia wala hayakuingia katika moyo wa binadamu mambo amabyo Mungu aliwaandalia wampendao."

Isaya alitufafanualia vipi kuhusu mbinguni? Imeandikwa, Isaya 65:21-23 "Na watajenga nyumba na kukaa ndani yake watapanda mizabibu na kula matunda yeke hawatajenga akakaa mtu mwingine hawatapanda akala mtu mwingine maana kama siku za mti ndivyo ndivyo zitakavyo kuwa siku za watu wangu na wateule wangu wataifurahia kazi yamikono yao mda wa siku nyingi. Hawatajitaabisha kwa kazi bure wala hawatazaa kwa taabu kwa sababu hao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana na watoto wao pamoja nao."

Kutakuwa na amani hata katika wanyama. Imeandikwa, Isaya 65:25 "Mbwa mwitu na mwana kondoo watalisha pamoja na simba atakula majani kama ngo'mbe na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka hata dhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote asema Bwana."

Wasio jiweza wataponywa. Imeandikwa. Isaya 35; 5-6 "Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikie ya visiwi yatazibuliwa ndipo mtu aliye kilema atarukaruka kama kulungu na ulimi wake aliye bubu utaimba maana katika nyika maji yatabubujika na vijito jangwani.."

Mungu ataishi na watu wake, hapo ndipo mwisho wa kifo, mochozi na maumivu. Imeandikwa. Ufunuo 21:3-4 "Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema tazama maskani ya Mungu ipamoja na wanadamu naye atafanya maskani yake pamoja nao nao watakuwa watu wake naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwapo tena wala maombolezo wala kilio wala maumivi hayatakuwapo tena kwa kuwa mambo yakwanza yamekwisha kupita."