Home / Masomo ya Biblia / Mfadhaiko

Mfadhaiko

Mfadhaiko waweza kuondoka kwa kutafakari maandiko ya Mungu na kutazamia matokeo mema kwake. Imeandikwa Zaburi 42:6 "Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka, taka nchi ya jordani na mahermoni na toka kilima cha mizari."

Maombi ni ufunguo wa kutoa majonzi imeandikwa 1samweli 1:10 "Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake akamuomba Bwana akalia sana."

Ni vema kuhesabu mibaraka yako. Imeandikwa Zaburi 107:8-9 "Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, na maajabu yake kwa wanadamu. maana hushibusha nafsi yenye shauku na nafsi yenye njaa huijaza mema."

Kuimba na kumsifu mungu kwa weza kutoa huzuni imeandikwa Zaburi 34:1-3 "Nitanhimidi Bwana kila wakati, sifa zake zi kinywani mwangu daima. katika Bwana nafsi yangu itajisifu, wanyenyekevu wasikie wakafurahi. Mtukuzeni Bwana pamoja nami, natuliadhimishe jina lake pamoja."

Nyimbo za kikristo za weza kutoa huzuni imeandikwa Zaburi 33:1-3 "Mpigieni Bwana vigelegele enyi wenye haki, kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo Mshukuruni Bwana kwa kinubi kwa kinanda cha nyizi kumi mwimbieni sifa mwimbieni nyimbo mpya pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe."

Huzuni na hofu hazi dumu imeandikwa Zaburi 30:5 "Ee Bwana Mungu wangu nalikulilia ukaniponya... 5 maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, katika radhi yake mna uhai. huenda kilio huja kukaa usiku, lakini asubuhi huwa furaha."

Kutee amri za Mungu huleta imani kwa mwenye huzuni imeandikwa Zaburi 119:165 "Wana amani nyinyi waipendao sheria yako, wala hawana lakuwakwaza."