Ridhika

Nijambo gani linaloleta ridhaa? Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu na hukuwa kwa kuwa na maisha ambayo yanaambatana na maagizo ya Mungu. Imeandikwa katika Wafilipi 4:12-13 "Najua kudhiliwa tena najua kufanikiwa katika hali yo yote na katika mambo yo yote nimefundishwa kushiba na kuona njaa kwa kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."

Ridhaa hukuwa kwa unyenyekevu na kumwamini Mungu. Imeandikwa katika Zaburi 131:1 "BWANA, moyo wangu hauna kiburi wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, wala na mambo yashindayo nguvu zangu."

Ridhaa hukuwa kwa kujitoa kwa Kristo na mambo ya milele. Imeandikwa katika Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili kwa maana atamchukia huyu ama atashikamana na huyu hamuwezi kumtumikia Mungu na mali."

Kutamani huzuia ridhaa. Imeandikwa katika Kutoka 20:17 "Usitamani nyumba ya jirani yako; usitamani mke wa jirani yako wala mtumwa wake au mjakazi wake wala ng'ombe wake, wala punda wake wala cho chote alicho nacho jirani yako."

Kupenda mali ni kizuizi cha ridhaa. Imeandikwa katika 1Timotheo 6:9 "Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi na tamaa nyingi zisizo na maana zenye kudhuru ziwatosazo wanadamu katika upotovu na uharibifu."