Safi

Twawezaje kuwa na maisha safi?. Imeandikwa, Zaburi 119:9 "Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? kwa kutii, kulifuata neno lako."

Furaha iko katika moyo safi. Imeandikwa, Mathayo 5:8 "Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu."

Je mafikara yetu ya fikiriye mambo gain?. Imeandikwa, Wafilipi 4:8 "Hatimaye ndugu zangu mambo yo yote yaliyo ya kweli yo yote yaliyo staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi yo yote yenye kupendeza yo yote yenye sifa njema, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote yatafakarini hayo."

Ni nani atakaye simama mbele za Mungu?. Imeandikwa, Zaburi 24:3-4 "Ni nani atakaye pnda katika mlima wa Bwana? ni nani atakaye simama katika patakatifu pake? mtu aliye na mkono safi na moyo mweupe asiyeinua nafsi yake kwa ubatili wala hakuapa kwa hila."

Kuwa safi ni kuwasaidia watu wenye shida. Imeandikwa, Yakobo 1:27 "Dini iliyo safi isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na dunia pasipo mawaa."

Mtu husikia na kuona anacho kitafuta. Imeandikwa, Tito 1:15 "Vitu vyote ni safi kwa hao waliyo safi lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi na nia zao pia."

Chagua marafiki walio wema na wenye mioyo safi. Imeandikwa, 2Timotheo 2:22 "Lakini zikimbie tamaa za ujanani, ukafuate haki na imani na upendo na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi."

Nilazima tuwe safi wakati Yesu anaporudi mara ya pili. Imeandikwa, 1Yohana 3:2, 3 "Wapenzi sasa tu wana wa Mungu wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa tutafanana naye kwa maana tutamwona kama alivyo. Nakila mwenye atumaini haya katika yeye hujitakasa kama yeye alivyo mtakatifu."