Twaweza kupata usalama kwake Yesu. Imeandikwa, 1Yohana 4:18 "Katika pendo hamna hofu lakini pendo lililo kamili huitupa hofu nje kama hofu ina adhabu na mwenye hofu hakukamishwa katika pendo."
Twaweza kuwa na usalama katiaka shida za ulimwengu huu. Imeandikwa, Zaburi 46:1-3 "Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso kwa kuwa hatutaogopa ijapobadili nchi ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari, maji yake yajapovuma na kuumuka ijapopepesuka milima kwa kiburi chake."
Twaweza kuwa na usalama tukifahamu yakuwa Mungu halali. Imeandikwa, Zaburi 121:2-4 "Msaada wangu ukatika Bwana. Aliyezifanya mbingu na nchi asiuashe mguu wako usongwe asisinzie akulindaye naam hatasinzia wala hatalala usingizi yeye aliyemlinzi wa Israeli."
Kuwa na usalama nikuwa na mafikara yaliyo atawi. Imeandikwa, Zaburi 112:7-8 "Hataogopa habari mbaya moyo wake u imara ukimtumaini Bwana. Moyo wake umedhibitika hataogopa, hata awaone watesi wake wameshindwa."
Tunahitaji usalama uliyoko katika Yesu Kristo. Imeandikwa, Yohana 6:39 "Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja bali ni mfufue siku ya mwisho."
Twahitaji kkuwa na usalama tukijua kuwa tuna tumaini ya kuishi milele. Imeandikwa, 1Yohana 5:11-12 "Na huu ndio ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika mwanawe. Yeye aliye naye mwana anao huo uzima; asiye naye mwana wa Mungu hana huo uzima."