Sifu

Nani wa msifu Bwana na vipi? Imeandikwa, Zaburi 150:1-6 "Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika anga la uweza wake msifuni katika matendo yake makuu msifuni kwa kadiri ya ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu msifuni kwa kinanda na kinubi; msifuni kwa matari na kucheza msifuni kwa sese na filimbi. Msifuni kwa matoazi yaliyayo msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya."

Kusifu ni kafara ya kiroho. Imeandikwa, Waebrania 13:15 "Basi kwanjia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani tunda la midomo iliungamayo jina lake."

Kusifu ni kumshukuru Mungu kwa zawadi ambazo ametupatia. Imeandikwa, Zaburi 103:2 "Ee nafsi yangu umhimidi Bwana wala usizisahau fadhili zake zote."

Msifu Mungu kwa msamaha wa dhambi na kujibu dua zetu. Imeandikwa, Zaburi 65:1-3 "Ee Mungu sifa zakulaiki katika sayuni, na kwako wewe itaondolewa nadhiri. Wewe usikiaye kuomba, wote wenye mwili watakujia. Ingawa maovu mengi yanamshinda, wewe utayafunika maasi yetu."

Aumbile nika kwaya imsifuye Mungu jinsi alivyo na atendayo. Imeandikwa, Zaburi 148, "Haleluya. Msifuni Bwana kutoka mbinguni; msifuni katika mahali palipo juu. Msifuni enyi malaika wake wote msifuni majeshi yake yote msifuni jua na mwezi; msifuni nyota zote zenye mwanga. msifuni enyi mbingu za mbingu. Nanyi maji mlioko juu ya mbingu. na vilisifu jina lake Bwana kwa maana aliamuri vikaumbwa. Amevidhibitisha hata milele na milele ametoa amri wala haitapita. Msifuni Bwana kutoka chini, enyi nyangumi na vilindi vyote. Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, upepo wa dhuruba ulitenda neno lake. Mlima na vilima vyote miti yenye matunda na mierezi yote. Hawayani na wanayama wafungwao, vitambaavyo na ndege wenye mbawa. Wafalme wa dunia na watu wote, wakuu na makadhi wote wa dunia. Vijana waume na wanawali wazee na watoto; na walisifu jina la Bwana maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake I juu ya nchi na mbingu. Naye amewainua watu wake pembe, sifa za watauwa wake wote, wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya."

Twamsifu Mungu kwa ukuu wake. Imeandikwa, Zaburi 21:13 "Ee Bwana utukuzwe kwa nguvu zako nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako."

Njia njem ya kumsifu Mungu ni kwa nyimbo. Imeandikwa, Zaburi 33:1-3 "Mpingieni Bwana vigelegele enyi wenye haki, kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni Bwana kwa kinubi kwa kinanda cha nyizi kumimwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe."

Sifu Mungu wakati wa mjonzi na shida. Imeandikwa, Zaburi 34:1-3 "Nitamhimidi Bwana kila wakati sifa zake zikinywani mwangu daima katika Bwana nafsi yangu itajisifu, wanyeyekevu wasikie wakafurahi mtukuzeni Bwana pamoja nami na tuliadhimishe jina lake pamoja."

Tumsfu Mungu kila siku. Imeandikwa, Zaburi 61:8 "Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima ili niondoe nadhiri zangu kila siku."

Tumsifu kwa kugeuza hofu kuwa furaha. Imeandikwa, Zaburi 30:11-12 "Uligeuze matanga yangu kuwa machezo; ulinivua ngunia ukanivika furaha. Ili utukufu wangu ukusifu wala usinyamaze. Ee Bwana Mungu wangu nitakushukuru milele."

Msifu Mungu kwa upendo wake na uzuri wake. Imeandikwa, Zaburi 107:8-9 "Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, na aajabu yake kwa wanadamu maana hushibisha nafsi yenye shauku na nafsi yenye njaa huijaza mema."