Home / Masomo ya Biblia / Upumbavu

Upumbavu

Kuto amini kuwa Mungu yupo ni upuzu imeandikwa Zaburi 14:1 "Mpumbavu asema moyoni hakuna mungu wame haribu matendo yao na kufanya chukizo hakuna atendaye mema."

Mambo ya mungu ni upuzi kwa asiye amini imeandikwa 1Wakorintho 2:14 "Basi wanadamu watabia ya asili haya pokei mambo ya Roho wa Mungu maana kwake huyo niupuzi wala hawezi kufahamu kwa kuwa yatambulika kwa jinsi ya rohoni."

Mpumbavu hana msimamo imeandikwa Medhali 29:11 "Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote bali mwenye hekima huizuia na kuituliza."

Mpumavu huongea bila kipimo imeandikwa Medhali 10:8 "Aliye na akili mwoyoni mwake atapokea agizo; bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka."

Medhali 17:28 "Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima akifumba midomo yake huhesabiwa ufahamu."