Urafiki

Urafiki haswa wahitaji kuaminiana Imeandikwa Mithali 17:17 "Rafiki hupenda sikuzote; na ndungu amezaliwa kwa siku ya taabu."

Rafiki mwema ni Yesu imeandikwa Yohana 15:15 " Siwaiti tena watumwa kwa maana mtumwa hajui atendalo Bwana wake lakini ninyi nimewaita rafiki kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu."

Jangua marafiki wanao mpenda Mungu na wenye mioyo misafi Imeandikwa 2 Timotheo 2:22 "Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki na imani na upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi."

Nimambo gani yanayo kufanyauwe rafiki mwema? imeandikwa Wafilipi 2:3-4 " Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno bali kwa unyenyekevu kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwqa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe bali kila mtu aangalie mambo ya mwengine."

Fitina uharibu urafiki Imeandikwa Mithali 16:28 " Mtu mshupavu huondokesha fitina; na mchongezi huwafarakanisha rafiki."

Rafiki ni mtu wa maana mtunze Imeandikwa Mithali 27:9-10 "Marhamu na manukato huufurahisha moyo; kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake Usimwashe rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako wala usiende nyumbani mwa ndungu yako siki ya msiba wako afathali jirani aliye karibu kuliko ndungu aliye mbali."

Rafiki atakwabiya jinsi mambo yalivyo hataiwapo ni machungu. Imeandikwa Mithali 27:6 " Jeraha utuwalo na rafiki ni amini bali kubusu kwa adui ni kwingi sana."