Uzinzi

Mungu ametuonya tusi zini. Katika kutoka 20:14 imeandikwa, "usizini".

Kumwacha mke wako au mume wako na kuoa mtu mwingine yaweza kuwa halali kwetu lakini kwa Mungu ni dhambi. Luka 16:18 inasema "Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini."

Kutamani mtu asiye mume au mke wako nikuzini katika Mathayo 5:27 -28 "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake."

Yesu alimchukulia vipi mwanamke aliyeshikwa akizini? Yohana 8:10-11 Inasema, " Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? je! hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? akamwambia, hakuna Bwana. Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Endazako; wala usitende dhambi tena."

Nimapenzi ya Mungu tusizini. Imeandikwa katika Wathesalonike wa kwanza 4:3 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, muepukane na usherati."