Home / Masomo ya Biblia / Wakristo wa uwongo

Wakristo wa uwongo

Yesu alituonya ya kuwa siku za mwisho kutakuwa na makristo wa uongo na kujifanya wakombozi wa ulimwengu huu. Imeandikwa, Mathayo 24:4-5 "Yesu akajibu akasema angalieni mtu asiwandangaye kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni kristo nao watadanganyika wengi."

Yesu alisema dalili yasiku zamwisho ni makristo wa uongo. Imeandikwa, Mathayo 24:23-26. "Wakati huo mtu akiwaambia tazama kristo yuko hapa au yuko kule msisadiki maana watatokea makristo wauongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza yamkini hata wateule. Tazama nimekwisha kuwaoya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani msitoke; yumo nyumbani msisadiki."

Paulo aliwaonya watu kuhusu mitume wauongo wasio hubiri Yesu wabibilia. Imeandikwa, 2Wakorintho 11:3-4 "Lakini na chelae kama yule nyoka alivyo mdanganya Hawa kwa hila yake asije akawaharibu fikara zenu mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri Y esu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri au mkipoke roho nyingine msiyoipokea au injili nyingine msiyo ikubali mnatenda vema kuvumilia naye."

Wakristo hao wengine wana mtumikia nani? Imeandikwa, 2Wakorintho 11:13-15 "Maana kama watu hao nimitume wa oungo watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mitume wakristo wala siajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru Basi si neno kubwa watumishi wake wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi yao."

Kabla yake Yesu kuja mara ya pili kutakuwa na onyesho la Kristo wa uongo. Imeandikwa, 2Wathesalonike 2:3-4 "Mtu waye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji usipokuja kwanza uleugeufu akafunuliwa yule mtu wa kuasi mwana wa uharibifu yule mpingamizi ajiinuae nafsi yake juu ya kila kiitwasho Mungu amakuabudiwa amayeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu akijionyesha nafsi yake kanakwamba yeye ndiye Mungu."

Je? Mwisho wa kristo wauongo utakuwaje na tutawajua vipi? Imeadikwa 2Wathesalonike 2:8-10 " Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi abaye Bwana Yesu atamwaua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake yule ambaye kuja kwake ni mfano wa kutenda kwake shatani kwa uwezo wote na ishara ya ajabu za uongo na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea kwasababu hawakukubali kuipenda ile kweli wapate kuokolewa."

Jambo la kuhuzunisha ni kwamba wale wanao mfuata yule mpinga kristo wanadhani yakuwa wanaifanya kazi ya Mungu. Imeandikwa, Mathayo 7:22-23 "Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa njina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi ndipo nitawaambia dhahiri sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu."