Mungu hutimiza ahadi zake. Imeandikwa katika 2Wakorintho 1:19-20 "Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yaani mimi na Silwano na Timotheo hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa sisi."
Mungu hazirudishi ahadi zake au kuzibadilisha. Imeandikwa katika Zaburi 89:34 "Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno lililotoka mdomoni mwangu."
Hakuna mojawapo ya ahadi za Mungu ambazo hazijatimika. Imeandikwa katika Yoshua 23:14 "Angalieni mimi nimekwenda njia ile waendayo watu wote wa ulimwengu...... Mungu wenu katika habari zenu yote yametimia kwenu hapana neno lo lote mlilopungukiwa."
Tumeahidiwa uzima wa milele. Imeandikwa katika 1 Yohana 2:25 "Nahii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani uzima wa milele."
Mungu aweza kufanya mambo yasiyowekana. Imeandikwa katika Luka 18:27 "Akasema yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa mungu." Tume ahidiwa moyo mpya na maisha mapya Imeandikwa Ezekieli 36:26 "Mimi nitawapa moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama." Ametuahidi kutusamehe dhambi zetu. Imeandikwa katika 1Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."
Ametuahidi tunda la roho. Imeandikwa katika Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la roho ni upendo, furaha amani, uvumilivu, utu wema fadhili uaminifu, upole, kiasi juu ya mambo kama hayo hakuna sheria." Ametuahi kututoa katika hofu. Imeandikwa katika Zaburi 34:4 "Nilimtafuta Bwana akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote."
Ameahidi wokovu. Imeandikwa katika Isaya 49:25, "... Kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu."
Ameahidi Roho mtakatifu Imeandikwa Luka 11:13 "Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho mtakatifu hao wamwombao?."
Atatutimizia mahitaji yetu. Imeandikwa katika Wafilipi 4:19, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu." Hatatunyima lililo jema. Imeandikwa katika Zaburi 84:11 "Kwa kuwa BWANA, Mungu ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu."
Ametuahidi hekima. Imeandikwa katika Yakobo 1:5 "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa." Mungu ametuahidi amani. Imeandikwa katika Isaya 26:3 "Utamlida yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini."
Mungu ametuahidi kutuepusha na majaribu. Imeandikwa katika 1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya binadamu; ila Mungu ni mwaminifu; hatawacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wakutokea ili muweze kustahimili."
Tumeahidiwa afya njema na tiba. Imo katika Biblia, Yeremia 30:17 "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA..."
Mungu ameahidi kutulinda na hatari na ajali. Imeandikwa katika Zaburi 91:10 "Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitaikaribia hema yako."
Biblia yatuahidi ya kwamba waliokufa watafufuka katika ufufuo. Imeandikwa katika Yohana 5:28-29 "Msistaajabie maneno hayo kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale walio fanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wao walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu."
Yesu ameahidi ya kwamba atarudi tena. Imeandikwa katika Yohana 14:2-3 "Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi; kama sivyo ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaanadalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo nanyi muwepo."
Ameahidi kukomesha vifo, maumivu na dhiki. Imeandikwa katika Ufunuo 21:4 "Naye atafuta kila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita."