Kifo

Tuna na paswa kufanya nini wakati mauti yako machoni mwetu? Ikiwa mungu yu pamoja nasi tusiwe na hofu imeandikwa Zaburi 23:4 "Naam nijapopita kati ya ponde lauvuli wa mauti sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja nami gongo lako na fimbo yako vyanifariji."

Kifo kinafanana vipi? Nikama usingizi. imeandikwa 1Wathesalonike 4:13 "Lakini ndugu hatutaki msijue habari za waliolala mauti msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini." pia Yohana 11:11-14 "Iliyasema hayo kisha baada ya hayo akawaambia, rafiki yetu Lazaro, amelala lakini nitakwenda nipate kumwamsha. Basi wale wanafunzi wakamwambia Bwana ikiwa amelala tapona lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake nao walidhani yakuwa ananena habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi Lazaro amekufa."

Danieli amesema nini kuhusu kifo? Imeandikwa Danieli 12:2 "Tena wengi wahao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka wengine wapate uzima wa milele wengine aibu na kudharauliwa milele."

Je? walio kufa wanajua lolote? Imeandikwa Mhubiri 9:5-6, 10Kwa sababu walio hai wanjua ya kuwa watakufa lakini wafu hawajui neno lolote wala hawana ijara tena maana kumbukumbu lao limesahauliwa mapenzi yao namachukio yao na husuda yao imepotea yote pamoja wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua, lolote mkono wako utakapolipata kulifanya ulifanye kwa nguvu zako kwa kuwa hakuna kazi wala shauri wala maarifa wala hekima huko kuzimu uwendako wewe."

Kifo sio mwisho! Imeandikwa Isaya 26:19 "Wafu wako wataishi maiti zako zitafufuka amkeni kaimbe ninyi mnao kaa mavumbini kwa maana umande wako nikama umande wa mimea nayo ardhi itawatoa waliokufa."

Yesu ametuhaidi nini kuhusu kifo? imeandikwa Hosea 13:14 "Nitawakomboa na nguvu za kaburi nitawaokoa na mauti ewe mauti yawapi mapigo yako? Ewe kaburi ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafishwa na macho yangu."

Ufufuwaji uko katika nguvu za mungu imeandikwa 1Wakorintho 15:21-22 "Maana ya kuwa mauti ili letwa na mtu kadhalika na kiyama ya wafu italetwa na mtu kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa kadhalika na katika kristo wate wanahuishwa."

Mungu alimpa mwanawe kwa sababu gani? imeandikwa Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenada ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ila kila amwaminiye asipotee bali awena uzima wamilele."

Watu wema na wabaya watafufuliwa siku ya kiama imeandikwa Yohana 5:28-29 "Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote walio makaburini wataisikia sauti yake nao watatoka wao waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima na wale walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu".

Waaminifu watafufuliwa yesu akirudi mara ya pili imeandikwa 1Wathesalonike 4:16-18 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbiguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya mungu nao walio kufa katika kristo watafufuliwa kwanza kisha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo."

Tutafanana vipi baada ya ufufuo? Imeandikwa Wafilipi 3:20-21 "Kwa maana sisi wenyeji wetu uko mbinguni kutoka huko tunamtazamia mwokozi Bwana wetu yesu kristo atakaye ubadili mwili wetu wa unyonge upate kufanana na mwili wake wa utukufu kwa uweza ule ambao kwa huo uweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake."

Watakatifu wataishi mdagani? imeandikwa Luka 20:36 "Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo."

Wenye dhambi wta ngoja kwa mda gani kabla ya kiama? imeandikwa Ufunuo 20:4-5, 9 "Kisha nikaona vitu vya enzi wakaketi juu yake nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya uchuhuda wa Yesu... Hao walio wafu salia hawakuwa hai hataitimie ile miaka elfu,... 9 Moto ukachika toka juu mbiguni ukawateketeza."

Wenye dhambi ni nani? imeandikwa Ufunuo 21:8 "Bali waoga, wasioamini, wachukizao, wauwaji, wazinzi, wachawi, waabuduo sanamu, na waongo sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti, hiyo ndiyo mauti ya pili."