Je? Tufanyeje tunaposikia kama kukata tamaa? Tumwambie Mungu jinsi tunavyo sikia Imeandikwa Zaburi 13:1 "Ee Bwana hatalini utanisahau hata milele? hata lini utanifisha uso wako?."
Mungu ametuahidi nuvu tunapo hitaji Imeandikwa Wakolosai 1:11-12 "Mkiwezeshwa kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha mkimshukuru Baba aliyewastahilisha kupokea sehemu ya uridhi wa watakatifu katika nuru."
Kukataa tamaa hutufanya tukakosa mema ambayo Mungu ametuhaidi. imeandikwa 2Wakorintho 4:16-17 "Kwa hiyo hatulegei bali ijapokuwa utu wetu wandani unafanywa upiya siku kwa siku, maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya muda wa kitambo tu yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana."
Wakati roho zetu zina tushukumu tusikate tamaa imeandikwa 1 Yohana 3:19, 20 "Katika hili tufahamu ya kwamba tu wa kweli nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, ikiwamioyo yetu inatuhukumu kwa maana mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote."