Lishe

Ni aina gani ya vyakula vilivyo pewa wanadamu hapo mwanzo? Imeandikwa Mwanzo 1:29 "Mungu akasema tazama nimewapa kile mche utoao mbengu ulio juu ya uso wa nchi yote pia na kila mti ambao matunda yake yana mbegu vitakuwa ndivyo vyakula vyenu."

Baada ya gharika Mungu alisema nini kuhusu vyakula. Imeandikwa Mwanzo 9:2-4 "Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi nakuwahofu na kila ndege wa angani : pamoja ni vitu vyote vilivyojaa katika ardhi na samaki wote wa baharini vimetiwa mikononi mwenu. kile kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyo wapa mboga za majani. Bali nyama pamoja na uhai yani damu yake msile."

Iliwabidi watu wawe waangalifu kuhusu vyakula walivyo paswa kula. Imeandikwa Walawi 11:47 "Ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi." (soma kitabu cha mambo ya walawi 11 kwa maelezo zaidi).

Vyakula hivi havikuwa vya wana waisraeli maagizo haya yalikuwa kitambo kabla ya Ibrahimu Imeandikwa Mwanzo 7:1, 2 "Bwana akamwamia Nuhu ingia wewe na jamaa yako yote katika safina kwa maana nime kuona wewe u mwenye haki mbela zangu katika kiza hiki kila wanya walio safi ujitwalie saba saba mume na mke na katika wanya wasio safi wawili wawili mme na mke."

Huu uwamuzi wa vilivyo safi na visivyo safi utaendelea hadi mwisho wa nyakati. imeandikwa Isaya 66:15, 17 "Maana Bwana atakuja na moto na magari yake ya vita kama upepo wa kisalisali ili atoe malipo ya gadhbu yake kwa moto uwakao na maonyo yake kwa miali ya moto. Watu wale wajitakasao na kujisafisha katika bustani nyuma yake aliye katikati wakila nyama ya nguruwe na machukizo na panya wata koma pamoja asema Bwana."

Danieli alitoa mfano upi wa malazi? imeandikwa Danieli 1:8 "Lakini danieli aliazimu moyoni mwake hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme wala kwa divai aliyokunywa basi akamwomba yule mkuu wa matoashi ampe ruhusa asijitie unajisi."

Alikula nini? imeandikwa Danieli 1:12 "Tafadhali utujaribu sisi watu mishi wako mda wa siku kumu; na watupe mtama tule na maji tunywe."

Kwanini tunapaswa kuwa na uwangalifu katika malazi yetu? imeandikwa 1Wakorintho 10:31, "Basi mlapo ua mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."