Maamuzi

Kabla huja fanya uwamuzi sharti uwe na uhakika. imeandikwa Methali 18:13 "Yeye ajibuye kabla hajasikia, ni upumbavu na aibu kwake.

Kabla hujafanya uamuzi nivema kufungua mawazo yako kwa mambo mapia. Imeandikwa Methali 18:15 "moyo wamwenye busara hupata maarifa; na sikio lamwenye hekima hutafuta maarifa."

Kabla hujafanya uwamuzi nivema kisikiliza pande zote za wateti au habari. Imeandikwa Methali 18:17 "Ajiteteaye kwa huonekana kuwa ana haki; lakini jirani yake huja na kumchunguza."

Wakati uamuzi umekuwa mgumu, Mungu ata kusaidia. Imeandikwa Yakobo 1:5 "Lakini mtu wakwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei, naye atapewa. Ila aombe kwa imani pasipo shaka yo yote maana mwenye shaka nikama wimbi labahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asithani ya kuwa atpokea kitu kwa mungu."

Umwamini mungu pekeyake Imeandikwa Methali 3:4-6 " Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, mbele za mungu na mbele ya wanadamu. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitengemee akili zako wewemwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako."

Maombi husaidia kufanya uwamuzi bara imeandikwa Luka 6:12 "Ikawa sikuiele aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usuku kucha katika kumwomba mungu."

Mungu husaidi mtu myenyekevu kuwaza kufanya uwamuzi. Imeandikwa Zaburi 25:9 "Wenye upole atawaongoza katika hukumu, wenye upole atawafundisha njia yake."