Home / Masomo ya Biblia / Malakika

Malakika

Malaika ni nani? Imo katika Biblia, Waebrania 1:14, Je? Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Kuna malaika wangapi? imeandikwa ufunuo 5:11 "Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai na za wale wazee, na hesabu yao ilikua elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,"

Je? malaika ni wa kiwango cha juu kuliko wanadamu? Imo katika Biblia, Zaburi 8:4-5 "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? umemfanya mdogo punde kuliko malaika; umemvika taji ya heshima."

Malaika aweza kutokea katika mfumo wa watu wa kawaida. Imo katika Biblia, Waebrania 13:2 "Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wame wakaribisha malaika pasipo kujua."

Ni nani kiongozi wa malaika? Imo katika Biblia, 1 Petro 3:22 " Naye yuko mkono mwa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiwa chini yake."

Malaika nikama washungaji wakipekee, imeandikwa Mathayo 18:10 " Angalieni msidharau mmoja yapo ya wadogo hawa; kwa maana na waambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote hutazama uso wa baba yangu aliye mbinguni."

Malaika hutu Linda. imeandikwa Zaburi 91:10-11. "Mabaya hayata kupata wewe, wala tauni haitakaribia hema yako. kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote."

Malaika wata kuondoa kwenye shida imeandikwa zaburi 34:7 Malaika wa bwana hufanya kituo, akiwazungukia wamshao na kuwaokoa."

Malaika huchukua amri za Mungu Imeandikwa Zaburi 103:20-21, " Mhidimu BWANA enyi malaika zake, ninyi mlio hodari mtendao neno lake, mkiisikiliza sauti ya neno lake. Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake."

Malaika hulieneza neno la Mungu Imeandikwa Luka 2:9-10 "Malaika wa BWANA akawatokea gafula utukufu wa BWANA ukawang'aria pande zote wakaingiwa na hofu kuu malaika akawaambia msiogope; kwa kuwa mimi nime waletea habari njema ya furaha kuu itakayo kuwa kwa watu wote."

Malaika watakuwa na kazi gani atakapo kuja yesu mara ya pili? imeandikwa Mathayo 16:27 "Kwa sababu mwana waadamu atakuja katika utukufu wa baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake." 24:31 " naye ata watuma malika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao wata wakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu mbingu mpaka mwisho huu."

Mashetani walitoka wapii? Imeandikwa ufunuo 12:9 "yule joka akatupwa yule mkubwa, nyoka wazamani aitwaye ibilisi na shetani audaganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa wote pamoja naye."

Je? malaika washetani wana mvuto gani katika maisha ya wanadamu? imeandikwa Waefeso 6:12 "kama kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wagiza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."

Je? Mwisho wa shetani na malaika wake utakuwa vipi? Imeandikwa Mathayo 25:41 "Kisha na atawaambia na wale walioko mkono wakushoto, ondokeni kwangu mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliyo wekewa tayari ibilisi na malaika zake."