Home / Masomo ya Biblia / Serikali

Serikali

Wenye malaka wata mjibu Mungu. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 17:18-19 "Tena naiwe zamani, aketipo juu ya kiti cha ufale wake ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo kufuatia hicho kilicho mbele ya makuhani walawi. Na awe nayo asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kumcha bwana Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi kwa kuyafanya."

Wenye madaraka wapaswa kuwachagua viongozi wema. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 16:18-19 "weka waamuzi na maakida katika malango yako yote akupayo Bwana, Mungu wako kwa hesabu ya kabila zako na wawaamue watu kwa maamuzi ya haki usipotoe waamuzi wala usipendelee uso wa mtu wala usitwae rushwa kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili na kugeuza dawaa ya wenye haki."

Lazima tuwaheshimu viongozi kwa kuwa Mungu amewashagua wawe kwenye uongozi. Imeandikwa, Warumi 13:1-4 "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu kwa kuwa hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo imeamriwa na Mungu hivyo amwesiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu nao washindanao watajipatia hukumu kwa kuwa watawalio hawatishi watu kwa sababubya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. basi wataka usimwogope mwenye mamlaka? fanya mema nawe utapata sifa kwake. kwa kuwa yeye nimtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema lakininufanyapo mabaya, ogopa kwa maana hauchukui upanaga bure kwa kuwa ni mtuishi wa Mungu mlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu."

Wakristo wanapaswa kusaidia viongozi inapowezekana. Imeandikwa, Titu 3:1 "Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka na kutii na kuwatayari kwa kazi njema."

Kumtii Mungu ni vema kuliko kumtii mwanadamu. Imeandikwa, Matendo ya mitume 5:29 "Perto na mitume wakajibu wakisema, imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu."

Mungu alitupa fano wema wa kulipa kodi. Imeandikwa, Mathayo 17:27 "Lakini tusije tukawakwaza, enda baharini ukatupe ndoana ukatoa samaki yule azukaye kwanza na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli uchukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako."

Nivema wakristo kulipa kodi. Imeandikwa, Warumi 13:5-7 "Kwa hiyo nilazima kutii si kwa sababu ya ile ghadhabu tu ila kwa sabau ya ile dhamiri kwa sabu hiyo tena mwalipa kodi kwa kuwa hao ni wahudumu wa Mungu wakidumu katika kazi iyo hiyo wapeni wote haki zao mtu wakodi, kodi mtu waushuru ushuru astahiliye hafu, hofu astahiliye heshima heshia.",