Ubatizo

Ni tendo gani lilo na uhusiano wa karibu zaidi na kuamini injili? Imeandikwa katika Marko 16:15-16 "Akawaambia enendeni ulimwenguni mwote mkahubiri injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa."

Wakati watu walipoamini wakati wa pentekosti Petero aliwaagiza wafanye nini? Imeandikwa katika Matendo ya mitume 2:38. "Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu, mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kile kipawa cha Roho mtakatifu."

Ubatizo una mfano upi? Imeandikwa katika Matendo ya mitume 22:16 "Basi sasa unakawilia nini? Simama, ukabatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake."
Ni aina ngapi za ubatizo tunazofunzwa katika Biblia? Imeandikwa katika Waefeso 4:5 "Bwana mmoja, imani mmoja, ubatizo mmoja."

Ubatizo huo unaelezwa vipi? Imeandikwa Warumi 6:2-7. "Hasha! sisi tulioifia dhambi tutaishije katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake. Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake kusudi kama Yesu alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba vivyo hivyo tuenende katika upya wa uzima."
Nini kinachotendeka katika ubatizo wa Yesu? Imeandikwa katika Mathayo 3:16-17. "Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia, akamuona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake. Na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema huyu ni mwanangu, mpendwa wangu ninayependezwa naye."

Nikwa jina gani tunalo paswa kubatizwa nalo? Imeandikwa Mathayo 28:19 "Basi enendeni katika mataifa yote mkawafanye kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu." Filipo alimfanyia ubatizo wapi yule myunani? Imeandikwa katika Matendo ya mitume 8:36-39. "Wakawa wa kiendelea njiani wakafika pahali penye maji yule towashi akasema, tazama maji haya nini kinachonizuia nisibatizwe? Filipo akasema, ukiamini kwa moyo wako wote inawezekana; akajibu akasema naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu, akaamuru lile gari lisimame wakatelemka wote wawili majini Filipo na yule towashi naye akabatizwa, Kisha walipopanda kutoka majini Roho wa Bwana akamnyakuwa Filipo yule towashi asimwone tena. Basi alikwenda zake akifurahi."

Ni maandalio gani tunapaswa kufanya kabla hatujabatizwa? Imeandikwa katika Matendo ya mitume 8:12. "Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake."